Ujenzi wa Sehemu ya Mizani Umeanza DWASAL
Dodoma Washed Sand Limited imeanza rasmi ujenzi wa sehemu ya mizani katika eneo la mradi. Wahandisi pamoja na wafanyakazi wengine tayari wapo eneo la kazi wakisimamia na kuendelea na hatua za awali za ujenzi.
Kampuni ya Dodoma Washed Sand Limited (DWASAL) imeanza rasmi ujenzi wa sehemu ya mizani (weighbridge) katika eneo la mradi kama sehemu ya kuimarisha miundombinu na kuboresha utendaji wa shughuli za kampuni.
Kwa sasa wahandisi pamoja na wafanyakazi wengine wapo eneo la kazi wakisimamia na kutekeleza hatua za awali za ujenzi. Mradi huu unatarajiwa kusaidia katika kupima uzito wa malori yanayoingia na kutoka kwa usahihi zaidi pamoja na kurahisisha shughuli za usafirishaji wa mchanga na vifaa vingine.
DWASAL inaendelea kujitolea kuboresha huduma na kuwekeza katika miundombinu itakayosaidia kuongeza ufanisi na uwazi katika shughuli zake.